Sipendi ujinga na hawapendi ujinga … (Second installment)

Posted by Group Kenya on Tuesday, October 11, 2016 at 7:31 pm

1. Mlevi anapanda gari alafu conda anamuuliza, “na hii ulevi yako utaenda mbinguni kweli, “mlevi akamjibu, “kama mnaenda mbinguni simamisha gari nishuke Mimi naenda tu apa ngara. PIA MLEVI HAPENDI UJINGA!

2. Juzi neighbor yangu alikuja akaniambia nipunguze sauti ya radio anataka kulala.Jana akipika chapoo na mimi nkamwambia apunguze harufu ya chapati nataka kula ugali. Saa hii tuko kwa landlord tunaongea hio maneno. Ju sipendi ujinga.

3. Ushawahi katia mrembo sana mpaka anakushow uende kwao akuna mtu kufika unapata pia yeye hayuko……KUMBE HUYO MREMBO HAPENDI UJINGA.

4. Sasa polisi anatusimamisha eti juu number plate ya nyuma na ya mbele haifanani, alafu beshteangu anamuuliza kama uso yake na matako inafanana. Mi imebidi nicheke sai tuko central ndo napatiana simu, so nitakua mteja kiasi. Hata polisi kumbe hawatakangi ujinga.

5. Ex wangu amenicall kuitisha earphones zake, nmempelekea earphones nkachukua simu yangu. nmemwacha akiziconnect kwa radio. Hata mimi sipendangi ujinga.

6. Nimeenda hosi kupimwa ugonjwa, results kukam doc ananisho ati choo yangu ni mbaya….sai najenga ingine, sipendingi ujinga mimi.

7. After sex dem anakuambia umpee panty ilianguka chini ya bed, unapata ni mbili na hukumbuki yake ilikuwa colour gani. Hapo ndio unatambua ufisi pia haitakangi ujinga.

8. Nlitoka rave 3am juzi. Kufika Moi avenue taxi ya home inalipisha 1500 na basi ya kwenda Mombasa inalipisha 700, Nlienda Mombasa na 700 nkarudi na 700 na nkabaki na mia. Sitakangi ujinga mimi.

9. Jana, nilikutana na boy fulani akaniuliza mbona nimekunja uso. , nikamjibu, nataka kuiweka kwa Bag. Sababu mi sipendi ujinga.

10. Mtoi wa neighbour amenizoea sana. nikimtuma kitu kwa duka anakula tu. juzi nilimtuma mkate akaila, jana nikamtuma blue band akala. leo nimtuma super glue, saa hii haongei…ujinga sipendi!

Share: Twitter Facebook Google+

Leave a Reply

#Jokes, Ujinga

NEXT: »

PREV: «

  • RECENT ARTICLES ON GROUP KENYA